Loading...

CCM yashinda Umeya Kigamboni

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando.
Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi (CCM), Maabadi Hoja ameshinda umeya wa Halmashauri mpya ya Kigamboni baada ya kupata kura tisa dhidi ya tano za Celestine Maufi wa Chadema.


Uchaguzi huo umefanyika jana (Jumamosi ) katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julisu Nyerere kilichopo Kigamboni.

Meya mpya wa Kigamboni Maabadi Hoja (katikati) akizungumza na wanahabari baada ya kuchaguliwa leo kulia ni Naibu meya Amin Sambo na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Steven Katembo. 
Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Rachel Mhando amesema jumla ya kura zilizopigwa ni 15 na moja iliharibika. 

Mhando ambaye ni Katibu Tawala wa Kigamboni, amesema nafasi ya naibu meya imekwenda kwa Amin Sambo kutoka CCM aliyemshinda Ernest Mafimbo wa CUF chini ya Ukawa.



Source: Mwananchi
ZeroDegree.
CCM yashinda Umeya Kigamboni  CCM yashinda Umeya Kigamboni Reviewed by Zero Degree on 12/18/2016 12:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.