Loading...

Mchakato wa kuwashughulikia wasaliti ndani ya Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] waanza.

CCM imeanza mchakato wa kuwashughulikia wasaliti ndani ya chama hicho, walioisumbua kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Hatua hiyo ni miongoni mwa mambo ambayo Kamati Kuu ya CCM iliyoketi jana jijini Dar es Salaam ikiongozwa na mwenyekiti wake, Rais John Magufuli ilijadili ikiwa ni sehemu ya tathmini ya uchaguzi huo.

Tangu uchaguzi huo umalizike ambao mgombea wa CCM, Rais Magufuli aliibuka na ushindi wa asilimia 58.46 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyepata asilimia 39.97, madai ya kuwapo wasaliti waliomuunga mkono yalitawala na kuwekwa mikakati ya kuwashughulikia kupitia vikao.

Mbali na kusababisha ushindani mkali dhidi ya CCM, Lowassa aliyehama chama hicho baada ya kuenguliwa katika mchakato wa urais na kwenda Chadema, aliviwezesha vyama vinavyounda Ukawa kupata wabunge 116, idadi kubwa kuwahi kufikiwa tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.

ZeroDegree.
Mchakato wa kuwashughulikia wasaliti ndani ya Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] waanza. Mchakato wa kuwashughulikia wasaliti ndani ya Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] waanza. Reviewed by Zero Degree on 12/12/2016 01:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.