Loading...

Pep Guardiola: Sina mpango na Dembele.

KOCHA wa Klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, amesema hakuna mpango wowote wa yeye kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Celtic, Moussa Dembele, akisema kwamba taarifa za namna hiyo mara nyingi hutungwa na waandishi wa habari.

Akizungumza kabla ya mchezo wao wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia M’gladbach, Guardiola alisema katika kipindi hiki kifupi alichokaa City, amepata taarifa za yeye kuwataka takribani wachezaji 100 hadi sasa kutoka kwenye vyombo vya habari, hivyo hana mpango wa kumnyakua straika huyo anayefanya vema Celtic kwa sasa.

Mshambuliaji wa klabu ya Celtic, Moussa Dembele.

ZeroDegree.
Pep Guardiola: Sina mpango na Dembele. Pep Guardiola: Sina mpango na Dembele. Reviewed by Zero Degree on 12/09/2016 04:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.