Loading...

PSG yapiga hodi Liverpool kwa mara nyingine tena kutafuta saini ya Coutinho.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa, Paris Saint-German (PSG) imejipanga kuhakikisha inamng’oa kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho baada ya msimu uliopita kushindwa kumsajili kutokana na dau lao kukataliwa na Liverpool.

Mtandao wa Express wa Uingereza umesema kuwa PSG wametenga Pauni Milioni 40 ili kumpata Countinho ikiwa ni dau mara mbili ya dau la kwanza ambalo walitaka kulitumia kumsajili Coutinho la Pauni Milioni 22.

Lakini licha ya dau hilo kuonekana kuwa kubwa lakini bado PSG inakumbana na ushindani kutoka kwa vilabu vingine duniani kama Barcelona na Bayern Munich ambazo zote zinaonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye uraia wa Brazil.

Coutinho mwenyewe kwa sasa yupo nje ya uwanja kutokana na kukabiliwa na jeraha la kifundo cha mguu wa kulia ambapo alitarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki saba na kurejea dimbani mwezi Januari mwakani lakini hivi karibuni alinukuliwa akisema kuwa anatamani kucheza mchezo wa Desemba, 31 dhidi ya Manchester City.

ZeroDegree.
PSG yapiga hodi Liverpool kwa mara nyingine tena kutafuta saini ya Coutinho. PSG yapiga hodi Liverpool kwa mara nyingine tena kutafuta saini ya Coutinho. Reviewed by Zero Degree on 12/26/2016 02:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.