Loading...

Tatu bora wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji bora Afrika watajwa.

Mshambuliaji na winga wa Algeria, Riyad Mahrez.
Mshambuliaji raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, mshambuliaji na winga wa Algeria Riyad Mahrez na winga wa Senegal Sadio Mané wameingia kwenye orodha ya wachezaji watatu bora wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika.

Wachezaji hao watatu wamefika hatua hiyo baada ya kupigiwa kura na makocha na wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya soka vilivyokuwa chini ya CAF, kamati za vyombo vya habari, kamati za soka na ufundi na wataalamu wa habari. Mohamed Salah na Slimani hawajafanikiwa kuingia katika hatua hii.

Mshambuliaji raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang.

Winga wa Senegal Sadio Mané.
Kwa mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani, golikipa wa Uganda Dennis Onyango na Mzimbabwe Khama Billiat na mchezaji wa Zambia kiungo Rainford Kalaba wameingia.

Washindi watatangazwa kwenye tuzo hizo maarufu kama Glo-CAF Awards Gala siku ya Alhamis, 5 January 2017 jijini Abuja, Nigeria.

Wanaowania Tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika
  • Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
  • Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)
  • Sadio Mané (Senegal & Liverpool)
Wanaowania Tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.
  • Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
  • Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns)
  • Rainford Kalaba (Zambia & TP Mazembe)
ZeroDegree.
Tatu bora wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji bora Afrika watajwa. Tatu bora wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji bora Afrika watajwa. Reviewed by Zero Degree on 12/24/2016 02:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.