Loading...

Trump atoa onyo kwa Kampuni zinazotaka kuondoka nchini Marekani.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amezionya kampuni dhidi ya hatua kali iwapo zitaondoka Marekani.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amezionya kampuni dhidi ya hatua kali iwapo zitaondoka Marekani.

Alikuwa akizungumza katika jimbo la Indiana ambapo alijisifu kwa kunusuru kazi 1000 katika kampuni ya Carrier Corp ambayo ilikuwa inapanga kuhamia Mexico.

Bw Trump sasa yuko katika jimbo la Ohio kuanza ziara ya kutoa shukrani kwa wafuasi wake.

Kiongozi huyo aliunga mkono mazungumzo na kampuni ya Carrier Corp kama mfano wa vile atakavyoshirikiana na wafanyibiashara wengine wanaotaka kuhamia mataifa mengine.

''Tutakuwa na hali ambapo wataelezwa kwamba tutawachukulia vyema na pia kutakuwa na hatua kali dhidi yao'',alisema.

''Watalipishwa kodi za viwango vya juu katika mpaka iwapo wanataka kuondoka''.

Pia aliahidi mpango wake wa kampeni wa kupunguza kodi miongoni mwa biashara nchini Marekani.

ZeroDegree.
Trump atoa onyo kwa Kampuni zinazotaka kuondoka nchini Marekani. Trump atoa onyo kwa Kampuni zinazotaka kuondoka nchini Marekani. Reviewed by Zero Degree on 12/03/2016 11:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.