Loading...

18% ya wakazi mkoani Iringa hawajui kusoma na kuandika

Naibu wa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Eng. Stella Manyanya amesikitishwa na kiwango cha hali ya kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu (illiteracy rate) katika Mkoa wa Iringa, ambayo ni asilimia 18.

Mkoa wa Iringa una jumla ya watu 941,238 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.

Eng. Manyanya aliyasema hayo juzi wakati ya ziara yake ya ufuatilialiaji wa vituo vya elimu nje ya mfumo rasmi, vituo sitiri na elimu ya watu wazima, mkoani Iringa.

Alisema kuwa takwimu hizo za kuongezeka watu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu zinahitaji juhudi za Serikali ili kufikia malengo ya kimataifa.

Alisema kuwa anatamani kuona katika sensa ya watu na makazi inayokuja fungu la watu wasiojua kusoma na kuandika mkoani Iringa na kwa nchi nzima linapungua.

Wakati wa ziara hiyo eng. Manyanya litembelea shule za msingi za Mwaya, Tumaini, Ikuvala, Mtua, Kilalakidewa na Ibumu zote za wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.

Akiongea na wananchi wa kijiji cha kilalakidewa kata ya Ibumu kitongoji cha Vigulu, katika mkutano wa hadhara, Naibu Waziri wa Elimu aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanaandikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule ili kupunguza tatizo la watu wasiojua kusoma na kuandika.

Awali, mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalla akitoa taarifa ya wilaya yake kwa naibu Waziri wa Elimu, alisema kuwa wilaya ina jumla ya watu wazima 10,373 wakiwemo wanaume 3,892 na wanawake 6,482 ambao hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Alisema kuwa taarifa hiyo ni kwa mujibu wa takimwu zilizokusanywa na idara ya elimu katika kipindi cha mwaka 2016 mwezi Oktoba.

Mkuu wa wilaya huyo alisema kuwa atahakikisha wilaya yake inatekeleza jukumu la kutoa elimu kwa watu wote na kuhakikisha kuwa kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapata fursa ya elimu.

Wilaya ya kilolo ina jumla ya vituo tisa (9)vya mpango wa elimu ya msingi kwa walioikosa (MEMKWA) vyenye jumla ya wanafuzi 198 kati yao wavulana 121 na wasichana 77.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa elimu wa mkoa wa Iringa, Richard Mfugale kwa niaba ya Katibu Tawala wa mkoa, asilimia kuwa mkoa wa unaendesha programu za elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.

Alisema kuwa mkoa una jumla ya vituo vya MEMKWA 18 vyenye jumla ya wanafunzi 338 kati ya hao wavulana 205 na wasichana ni 133.

Mfugale alisema kuwa utoaji wa elimu ya watu wazima unakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wake.

Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni honoraria kwa wawezeshaji wa program na kusababisha wawezeshaji kuacha na kutafuta shughuli zingine.

Changamoto zingine ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na uhaba wa rasilimali fedha kwa ajili ya ufuatiliaji wa programu hiyo ya MEMKWA.

Alisema kuwa changamoto nyingine ni ufinyu wa bajeti ya ufuatiliaji wa programu hiyo katika kitengo cha elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.

Wakati huohuo, naibu waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Eng. Stella Manyanya amesikitishwa na hali ya miundombinu ya madarasa ya wanafunzi wa MEMKWA katika baadhi ya shule za msingi wilayani Kilolo, mkoani Iringa isiyoridhisha.

Aidha, Eng. Manyanya alitoa rai kwa wakuu wa shule nchini wanatakiwa kuwa na madarasa ya MEMKWA katika shule zao na kuagiza kuachana na walimu wa kujitolea wanaofundisha madarasa hayo.

Alisema kuwa baadhi ya shule zina walimu wakutosha hivyo watumie rasilimali watu zilizopo kufundisha madarasa ya MEMKWA ili kupunguza ubaguzi kwa wanafunzi wa MEMKWA kwa kuwaita wanafunzi wa elimu nje ya mfumo rasmi, bali waitwe wanafunzi.

Source: Dewji Blog
ZeroDegree.
18% ya wakazi mkoani Iringa hawajui kusoma na kuandika 18% ya wakazi mkoani Iringa hawajui kusoma na kuandika Reviewed by Zero Degree on 1/22/2017 12:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.