Loading...

Afcon: Ghana yailaza Uganda kwa ushindi wa bao 1 bila [Video]

Andre Ayew alifunga bao la pekee la mechi dhidi ya Uganda katika mechi ya ufunguzi ya kundi D katika michuano ya kombe la bara Afrika linaloendelea nchini Gabon.

Winga huyo wa klabu ya West Ham alifunga bao la penalti kunako dakika ya 32 baada ya nahodha Asamoah Gyan kuvutwa katika eneo la hatari.

Ghana pia ilitishia kupitia vichwa viwili vya Gyan ,huku Ayew na Christian Atsu wakimjaribu kipa wa Uganda Denis Onyango.

Uganda walikaribia lango la Ghana baada ya Faruku Miya kupiga mwamba wa goli lakini hawakuweza kusawazisha.

Uganda wanaocheza kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978 hawakuwa na bahati.

Cranes walitengeza fursa chache na walishindwa kuingia katika lango la Ghana ambao walifurahia kulinda lango lao.

Mchezo mwingine ulichezwa usiku wa jana, kati ya Mali dhidi ya Misri ambapo matokeo yalikuwa sare ya bila kufungana.

Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi za Kundi A, ambapo timu ya wenyeji Gabon itakuwa ikimenyana na Burkina Faso Saa 1:00 jioni na nyingine usiku kati ya Cameroon na Guinea - Bissau Saa 4:00
.



ZeroDegree.
Afcon: Ghana yailaza Uganda kwa ushindi wa bao 1 bila [Video] Afcon: Ghana yailaza Uganda kwa ushindi wa bao 1 bila [Video] Reviewed by Zero Degree on 1/18/2017 11:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.