Loading...

Alichojibu Rais Magufuli kwa DC aliyeomba kujiuzulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjibu Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora aliyeomba kujiuzulu wadhifa huo.

Katika majibu yake Rais Magufuli ameridhia uamuzi huo na kwamba uteuzi wa mtu mwingine atakayejaza nafasi hiyo utafanyika baadaye.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu bwana Gerson Msigwa imesema “Ombi la Bw. Gabriel Simon Mnyele aliyeomba kujiuzulu wadhifa wake wa Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora limekubaliwana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora itajazwa baadaye.”

Taarifa za kujiuzulu kwa Mkuu huyo wa wilaya zilianza kusambaa jana zikidai kuwa Mkuu huyo wa Wilaya aliaga katika Kamati ya Madiwani wa CCm, pamoja na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa halmashauri kuwa ameamua kuchia ngazi, bila kueleza sababu sababu za uamuzi huo.

Hata hivyo baadaye kulitokea utata baada ya kusambaa kwa taarifa za yeye kukanusha kufanya uamuzi huo, lakini sasa ni dhahiri kuwa Bw. Gabriel Simon Mnyele siyo mkuu wa wilaya hiyo tena.



ZeroDegree.
Alichojibu Rais Magufuli kwa DC aliyeomba kujiuzulu Alichojibu Rais Magufuli kwa DC aliyeomba kujiuzulu Reviewed by Zero Degree on 1/27/2017 08:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.