Loading...

Aliyekuwa Rais wa zamani wa Iran, Akbar Hashemi Rafsanjani afariki dunia.

Rais wa zamani wa Iran,  Hashemi Rafsanjani.
Rais wa zamani wa Iran, Ayatollah Ali Akbar Hashemi Rafsanjani, afariki dunia jana huko mjini Tehran akiwa na umri wa miaka themanini na mbili.

Kifo chake kimetangazwa na Televisheni ya Taifa ya Iran huku ikitajwa kuwa, kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza kutoa salamu za rambirambi za kifo cha rais huyo mstaafu.

Licha ya tofauti walizokuwa nazo viongozi hao, lakini kiongozi huyo wa dini amemtaja Rafsanjani kama mpambanaji.

Rafsanjani alikuwa akimuunga mkono rais wa sasa Hassan Rouhani ambaye amemsifu kuwa ni mwana mapinduzi mkubwa.

Kushoto ni Faezeh Hashemi Rafsanjani, mtoto wa marehemu Rafsanjani, akiwa na ndugu zake wakiomboleza.

Pamoja na mambo mengine, siku tatu za maombolezi zimetangazwa.

Ayatollah Rafsanjani aliwahi kuwa rais kati ya mwaka 1989 hadi 1997 na ameendelea kuwa na nafasi muhimu katika siasa za Iran.

ZeroDegree.
Aliyekuwa Rais wa zamani wa Iran, Akbar Hashemi Rafsanjani afariki dunia. Aliyekuwa Rais wa zamani wa Iran, Akbar Hashemi Rafsanjani afariki dunia. Reviewed by Zero Degree on 1/09/2017 10:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.