Loading...

Andy Carroll amponda Dimtri Payet kwa uamuzi wake

Kwa siku za karibuni habari ya kiungo wa West Ham, Dimitri Payet kutaka kuondoka klabuni hapo inaonekana kushika kasi hasa baada ya kocha wa timu hiyo kuweka wazi kuwa Payet hayupo tayari kuendelea kuichezea West Ham na anataka kuondoka.

Baada ya habari hizo za Payet kutaka kuondoka, mchezaji mwenzake wa West Ham, Andy Carroll ameponda uamuzi ambao Payet ameufanya na kusema kuwa hakuna mchezaji mkubwa kuliko klabu kiasi cha kufanya timu kushindwa kufanya jambo ambalo mashabiki wanataka kuliona.

“Sidhani kama kuna mchezaji bora kuliko klabu, hilo ndilo ninalo amini, meneja, wafanyakazi na mashabiki wote tunawaonyesha kuwa tupo pamoja wa kunatafuta alama tatu kwa ajili yao

“Kwa jambo ambalo lilikuwa likiendelea wiki hii na kila mtu akilizungumza, nilipokea simu nyingi na ujumbe mfupi na hilo lilikuwa hivyo kwa wachezaji wengine, ilikuwa ngumu na zaidi kwa watu wa karibu,” alisema Caroll.

Katika mchezo wa jana wa West Ham iliyowakaribisha Crystal Palace, Payet hakuwepo katika orodha ya wachezaji ambao wangecheza mchezo huo uliomalizika kwa West Ham kiushinda goli 3-0 kwa madai kuwa amekataa kucheza.

ZeroDegree.
Andy Carroll amponda Dimtri Payet kwa uamuzi wake Andy Carroll amponda Dimtri Payet kwa uamuzi wake Reviewed by Zero Degree on 1/15/2017 07:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.