Loading...

Busungu anavyoteswa na kesi ya Barabarani

YANGA imeendelea kumkosa mshambuliaji wake Malimi Busungu, ambaye bado anakabiliwa na kesi yake ya tuhuma za makosa barabarani itakayoendelea kuunguruma Januari 10 mwaka huu mjini Morogoro.

Busungu alitarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji ambao wangepewa nafasi kwenye kikosi cha kocha George Lwandamina kinachoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar, lakini kuibuka kwa kesi hiyo kumemkosesha straika huyo nafasi ya pekee ya kuonesha uwezo wake kwenye michuano hiyo.

Kutokana na kesi hiyo, Busungu amekuwa akisafiri mara kwa mara kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kwenye kesi hiyo jambo lilomfanya pia akose baadhi ya mazoezi ya pamoja na kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Nipo Dar es Salaam kwa sasa, siwezi kwenda Zanzibar mpaka kesi yangu imalizike. Nina imani Mungu akisaidia kesi hii itamalizika Jumanne na nitaweza kuungana na wenzangu ingawa nimechelewa sana,” alisema Busungu.

Busungu alikumbana na kesi hiyo baada ya kusababisha ajali wakati akitokea Morogoro eneo la Dakawa. Ni changamoto iliyomkumba katika kipindi hiki anachojaribu kupambana ili arudi kwenye kikosi cha kwanza chini ya Lwandamina ambaye hajaweza kukaa naye kwa muda mrefu tangu atue wiki chache zilizopita.


Source: Dimba
ZeroDegree.
Busungu anavyoteswa na kesi ya Barabarani Busungu anavyoteswa na kesi ya Barabarani Reviewed by Zero Degree on 1/09/2017 01:49:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.