Loading...

Magari ya Serikali yenye makosa sasa kutozwa faini

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga 
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema kumekuwapo na malalamiko ya kuwa magari ya Serikali yanapendelewa na hivyo zitawekwa kamera katika barabara kuu ili kupiga picha magari yote na yenye makosa yataadhibiwa.

Kamanda Mpinga amesema hayo wakati wa mahojiano maalumu waandishi wa habari na kusema kuwa katika kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka jana, makosa yaliyotokea nchini ni milioni 1.9 huku Dar es Salaam ikiwa na theluthi ya makosa hayo. 

“Kamera hizo hazitajali kuwa ni gari ya Waziri, Serikali, wala Mpinga na zitapiga picha gari zote kama ilivyo kwa msemo wa kupanga ni kuchagua,” amesema.

Amesema kuwa makosa hayo yalitokana na ulevi, mwendo wa kasi, kupita katika taa nyekundu, kukatisha safari na kutokuvaa kofia ngumu.

ZeroDegree.
Magari ya Serikali yenye makosa sasa kutozwa faini Magari ya Serikali yenye makosa sasa kutozwa faini Reviewed by Zero Degree on 1/16/2017 12:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.