Loading...

Majibu ya ACT wazalendo kwa Hamphrey Polepole

Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole 

Chama cha ACT-Wazalendo, kimemjibu Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole kwa kumueleza kuwa kazi ya chama cha siasa ni kuhangaika na matatizo ya wananchi.

Jana, Polepole aliwataka wapinzani kuacha kutumia matatizo ya wananchi kujinufaisha kisiasa huku akitolea sakata la njaa na tetemeko la ardhi liliotokea Bukoba.

Akizungumza na wanahabari leo (Jumatano) katika Makao Makuu ya ACT-Wazalendo, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma kwa chama hicho, Ado Shaibu amesema kukabiliana na matatizo ya wananchi ndiyo mtaji sahihi wa kisiasa.

"Chama cha siasa lazima kishughulike na matatizo ya wananchi, kisichojishughulisha na matatizo ya wananchi kitakufa,"amesema Shaibu.





Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Majibu ya ACT wazalendo kwa Hamphrey Polepole Majibu ya ACT wazalendo kwa Hamphrey Polepole Reviewed by Zero Degree on 1/18/2017 06:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.