Loading...

Muda wa Ban Ki Moon kama Katibu wa umoja wa mataifa [UN] umekwisha.

Ban Ki-moon akamilisha muhula wake katika Umoja wa Mataifa ambapo amehudumu kama katibu mkuu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayestaafu, Ban Ki-moon, ameondoka makao makuu ya Umoja wa Mataifa , kwa mara ya mwisho baada ya muhula wake wa mwongo mzima.

Bwana Ban Ki-moon anamaliza kazi rasmi, mwaka mpya unapoingia.

Alisema atakuwepo katika Medani ya Times mjini New York, kuukaribisha mwaka, na kuadhimisha kumaliza kazi.

Allitoa lugha aliyokuwa katika hari ya utani, pale sliposema kwamba mamilioni ya watu watakuwa wakiangalia wakati akipoteza kibarua chake.

Nafasi yake inachukuliwa na waziri mkuu wa zamani wa Ureno, Antonio Guterres.

Bwana Ban anatarajiwa kurudi Korea Kusini, ambako kuna tetesi, kwamba huenda akagombea nafasi ya Rais Park Geun-Hye, ambaye anashtakiwa.

ZeroDegree.
Muda wa Ban Ki Moon kama Katibu wa umoja wa mataifa [UN] umekwisha. Muda wa Ban Ki Moon kama Katibu wa umoja wa mataifa [UN] umekwisha. Reviewed by Zero Degree on 1/01/2017 12:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.