Loading...

Mzee wa miaka 83 akutwa akiwa amekufa pembeni ya kaburi la mkewe

Mzee mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 83 amekutwa amekufa pembezoni ya kaburi la mke wake baada ya kujipiga risasi ya kichwa katika makaburi ya St. John yaliyopo katika kijiji cha Middle jijini New York, Marekani.

Mzee huyo ambaye alitambulika kwa jina la Robert Gallo alikuwa amekwenda eneo hilo kwa ajili ya kutembelea kaburi la mke wake lakini baada ya muda mlio wa risasi ulisikika na walinzi wa eneo hilo walipokwenda kuangalia nini kimetokea walimkuta akiwa amelala chini pembeni na kaburi la mke wake.

Msemaji wa makaburi ya St. John alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kwa mzee Gallo kupoteza maisha kwani walikuwa wamemzoea kumwona mara kwa mara kutokana na utaratibu ambao alikuwa amejiwekea wa kwenda katika kaburi la mke wake.

“Wafanyakazi wengi wa makaburi haya wanamjua vizuri, huwa anatembelea kaburi la mke wake mara kwa mara,” alisema msemaji wa makaburi hayo na kuongeza “Tumesikitishwa na jambo ambalo limetokea na tunamwombea yeye pamoja na familia yake.”

ZeroDegree.
Mzee wa miaka 83 akutwa akiwa amekufa pembeni ya kaburi la mkewe Mzee wa miaka 83 akutwa akiwa amekufa pembeni ya kaburi la mkewe Reviewed by Zero Degree on 1/28/2017 11:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.