Loading...

Schneiderlin kutimkia Klabu ya Everton

Manchester United imekubali kumuuza kiungo wa kati Morgan Schneiderlin kwa pauni milioni 22.

Sasa Morgan atajiunga na Everton.

Mfaransa huyo, 27, alinunuliwa na Manchester United kwa kitita cha pauni milioni 25 kutoka Southampton mwezi Julai 2015 chini ya ukufunzi wa Louis van Gaal.

Kufuatia ushindi wa Man U wa 2-0 dhidi ya Hull City, Morinho alisema: "naibu mwenyekti Ed Woodward ameniarifu kwamba mpango wa kumuuza unakaribia kukamilika"

Ameiwakilisha Man U mara 47, japo chini ya ukufunzi wa Jose Morinho msimu amecheza mara 8 pekee, mara tatu katika dimba la ligi kuu ya Uingereza.

Hayo yakiarifiwa, mshambuliaji Oumar Niasse, 26, wa Everton atahama kwa mkopo kuelekea Hull City japo makubaliano ya kibinafsi bado hayajaafikiwa.

Raia huyo wa Senegal alijiunga na Everton mwezi februari mwaka 2016 kwa kitita cha pauni milioni 13.5 kutoka Lokomotiv Moscow japo amechezea klabu hiyo mara saba pekee.

ZeroDegree.
Schneiderlin kutimkia Klabu ya Everton Schneiderlin kutimkia Klabu ya Everton Reviewed by Zero Degree on 1/11/2017 05:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.