Loading...

Yanga yaanza vyema mbio za kulitetea kombe la FA

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), wameanza vyema kulitetea taji lao kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ashanti United.

Mchezo huo uliochezwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku mlinda mlango Benno Kakolanya wa Yanga akiokoa mipira mingi ya hatari kwenye lango lake.

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Amis Tambwe ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa Msuva.

Dakika 37 Yanga walipata bao la pili kupitia kwa Thaban Kamusoko baada kuachia shuti kali nje ya kumi na nane lilomshinda mlinga mlango Rajabu Kahumbu.


Msuva alifunga bao la tatu dakika ya 53 kwa penati baada ya Seleman Sultan kumchezea vibaya Msuva na muamuzi Ahmad Kikumbo kuamuru penati ipigwe na winga huyo akaweka mpira kambani.

Dakika 61 Ashanti wanapata goli la kufutia machozi lililofungwa na Isack Hassan ambaye aliwazidi ujanja mabeki wa Yanga.

Yusuph Muhilu alikamilisha karamu ya magoli dakika ya 89 baada ya kufunga bao la nne kwa k umalizia krosi ya Emmanuel MartinYanga ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Amis Tambwe, Simon Msuva, Juma Mahadhi na kuwaingiza Matheo Anthoy, Emmanuel Martin na Yusuph Muhilu.

Kesho kutakuwa namchezo mwingine katika michuano hii katika ya Simba na Polisi Dar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

ZeroDegree.
Yanga yaanza vyema mbio za kulitetea kombe la FA Yanga yaanza vyema mbio za kulitetea kombe la FA Reviewed by Zero Degree on 1/21/2017 07:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.