Loading...

Farid Mussa apandishwa kikosi cha kwanza Tenerife

WINGA Farid Malik Mussa amepandishwa kikosi cha kwanza kwenye timu yake ya Deportivo Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.

Akizungumza jana na kwa njia ya mtandao kutoka Hispania, Farid alisema kuwa tangu wiki iliyopita ameanza kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha timu hiyo.



Alisema kuwa licha ya kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza, bado amekuwa akicheza kwenye kikosi cha pili cha timu hiyo kwenye mechi peke yake.

“Namshukuru Mungu hatimaye nimepandishwa kikosi cha kwanza, kwa sasa nacheza kwenye kikosi cha pili endapo kunakuwa na mechi tu.

Alisema amefurahishwa kufanya mazoezi na kikosi hicho cha kwanza na kwa sasa anapambana kuweza kupata namba.
Alisema taratibu ameanza kuzoea mazingira ya nchini humo na makocha wake wameanza kumuamini.

Faridi alijiunga na timu hiyo mwishoni mwa mwaka jana kwa mkopo wa muda mrefu akitokea kwenye kikosi cha Azam FC.


Source: Nipashe
Farid Mussa apandishwa kikosi cha kwanza Tenerife  Farid Mussa apandishwa kikosi cha kwanza Tenerife Reviewed by Zero Degree on 2/15/2017 02:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.