Loading...

Guardiola atoa ya moyoni juu ya kitendo cha mashabiki kumuandama kocha Arsene Wenger

Kitendo cha kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kuandikwa na kusemwa na wadau wengi wa soka kutokana na matokeo ambayo timu yake inayapata, kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameweka wazi kukerwa na jambo hilo.

Guardiola amesema kitendo anachofanyiwa kocha mwenzake sio cha kibinadamu na hakikubaliki mbele ya jamii kuwa wanamzungumza vibaya Wenger na hilo sio jambo la heshima kufanyiwa kocha ambaye tayari ameshafundisha timu kama Arsenal kwa zaidi ya miaka 15.

“Kwa jambo ambalo nilisikia ndani ya siku 10 zilizopita kutoka kwa watu, wachezaji wa zamani na waandishi wa habari jinsi wanavyomfanyia kwa mfano Arsene Wenger haikubaliki,” alisema Guardiola na kuongeza.

“Kwa mimi, na kwa kwazi yetu ilivyo sasa, hatuna heshima yoyote katika nafasi yoyote ambayo tunakuwepo. Jambo ambalo limetokea halikubaliki. Tunachukua maamuzi na unaweza kusema jambo lolote ambalo unajisikia kusema.”
Guardiola atoa ya moyoni juu ya kitendo cha mashabiki kumuandama kocha Arsene Wenger Guardiola atoa ya moyoni juu ya kitendo cha mashabiki kumuandama kocha Arsene Wenger Reviewed by Zero Degree on 2/20/2017 12:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.