Loading...

Hizi hapa Timu 3 za Ligi daraja la kwanza zilizopanda kucheza Ligi kuu ya Vodacom [VPL] msimu ujao

Timu ya Njombe Mji kutoka Mkoani Njombe imefanikiwa kupanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara msimu ujao 2017/18 baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 mbele ya Kurugenzi ya Mafinga mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Wambi mjini Mafinga.

Njombe Mji imekuwa timu ya tatu kupanda daraja na kukamilisha idadi ya timu kutoka ligi daraja kwanza zilizopanda kucheza VPL kwa msimu ujao ambazo ni Lipuli (Iringa), Singida United (Singida) na Njombe Mji (Njombe).

Wakati timu tatu zikipanda daraja kutoka ligi daraja la kwanza kwenda ligi kuu Tanzania bara, kuna timu tatu ambazo zimeshuka daraja kutoka ligi daraja la kwanza hadi ligi daraja la pili ambazo ni Kimondo SC (Mbozi), African Sports (Tanga) pamoja na Panone FC (Kilimanjaro).
Hizi hapa Timu 3 za Ligi daraja la kwanza zilizopanda kucheza Ligi kuu ya Vodacom [VPL] msimu ujao Hizi hapa Timu 3 za Ligi daraja la kwanza  zilizopanda kucheza Ligi kuu ya Vodacom [VPL] msimu ujao Reviewed by Zero Degree on 2/19/2017 02:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.