Loading...

Idara ya haki nchini Marekani yatetea marufuku iliyotolewa na Rais Donald Trump

Raia wa Yemen waliozuiwa kuingia Marekani na agizo hili wameanza kurudi nchini humo
Idara ya haki nchini Marekani imeitetea marufuku ya usafiri ya rais Donald Trump na kuitaka mahakama ya rufaa kuiruhusu kwa usalama wa taifa.

Taarifa ya kurasa 15 ilidai kwamba ilikuwa ni hatua ya halali kwa rais Trump na sio kuwapiga marufuku Waislamu.

Agizo hilo la rais liliwazuia kwa muda wakimbizi wote na wageni kutoka mataifa saba ya Waislamu.

Kesi ya kuikubali ama kuikataa marufuku hiyo imepangwa kusikizwa siku ya Jumanne.

Ombi hilo liliwasilishwa katika mahakama ya rufaa ya San Francisco baada ya agizo hilo la Trump kusitishwa na jaji wa mahakama ya kijimbo mjini Washington.

Jaji huyo alisema kuwa marufuku hiyo ni kinyume na katiba na inadhuru maslahi ya taifa hilo.

Kufuatia uamuzi huo raia kutoka mataifa saba ya Waislamu ikiwemo Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen walio na Visa halali waliweza kusafiri kuelekea Marekani.
Idara ya haki nchini Marekani yatetea marufuku iliyotolewa na Rais Donald Trump Idara ya haki nchini Marekani yatetea marufuku iliyotolewa na Rais Donald Trump Reviewed by Zero Degree on 2/07/2017 11:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.