Loading...

Kaseja atangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwezi Januari

KIPA wa Kagera Sugar ya Bukoba, Juma Kaseja.
KIPA wa Kagera Sugar ya Bukoba, Juma Kaseja, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa Januari imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.

Kaseja ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda wachezaji wengine wawili ambao walikuwa wanachuana.

Wachezaji ambao walikuwa wanashindana na Kaseja ni pamoja na mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mbarak Yusuph na Jamal Mtengeta wa Toto Africans ya jijini, Mwanza. 

Kufuatia kushinda tuzo hiyo, Kaseja atajinyakulia zawadi ya Sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wakuu wa Ligi ya Bara, Kampuni ya Simu za mikononi ya Vodacom.

Kipa huyo wa zamani wa Simba, Yanga, Moro United na timu ya Taifa (Taifa Stars) alijiunga na Kagera Sugar Desemba mwaka jana akitokea Mbeya City.

Kaseja ndiye kipa chaguo la kwanza la Kagera Sugar ambayo hivi karibuni ilipoteza mlinda mlango wake mwingine, David Burhani, aliyefariki dunia huku ikimsimamisha Hussein Shariff 'Cassilas' kutokana na kudaiwa kuihujumu timu hiyo katika mechi dhidi ya Yanga.
Kaseja atangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwezi Januari Kaseja atangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwezi Januari Reviewed by Zero Degree on 2/23/2017 12:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.