Loading...

Kuingia 'TOP 4' ni kazi ngumu sana, Jose Mourinho akiri.

HARAKATI za kuifikisha timu ya Manchester United kwenye ‘Top 4’ ya Ligi Kuu England msimu huu, zimeanza kuingiwa na hofu baada ya kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho, kusema ratiba ya mechi za makombe mengine huenda ikamvurugia harakati zake hizo.

Mchezo wa Kombe la FA baina yao na Wigan ulikuwa ni wa kwanza kati ya mechi saba za michuano minne ndani ya wiki nne ambazo zimemuweka Mourinho kwenye hofu ya kuikosa ‘Top 4’, kwani watakabiliwa na fainali ya EFL dhidi ya Southampton, mara baada ya kukamilisha mechi nyingine tano dhidi ya Hull City, Leicester, Watford na mechi mbili za 32 bora Ligi ya Europa dhidi ya St. Etiene.

“Tuna mtihani mzito hivi sasa, hatutakutana na Man City kama ilivyokuwa ratiba ya awali ya ligi na bado tuna mechi za Europa.

“Shida ni kwamba iwapo tutasonga mbele zaidi kwenye ligi ya Europa, huku tukicheza fainali na Southampton ambao watakuwa wamejiandaa vya kutosha, pia kama tukifuzu zaidi kwenye FA Cup, kuna mzunguko mwingine utafuatia hapo.

“Ni ngumu sana kwetu lakini ni vizuri tukisonga mbele,” alisema.
Kuingia 'TOP 4' ni kazi ngumu sana, Jose Mourinho akiri. Kuingia 'TOP 4' ni kazi ngumu sana, Jose Mourinho akiri. Reviewed by Zero Degree on 2/01/2017 06:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.