Loading...

Licha ya kufukuziwa sana na Chelsea, Verratti ameitaja klabu ambayo angependa kuhamia akiondoka PSG

KIUNGO mahiri wa klabu ya PSG, Marco Verratti amesema angependa zaidi kujiunga na Barcelona ya Hispania, huku ikijulikana wazi kwamba klabu ya Chelsea nayo inamhitaji kwa udi na uvumba.

Huenda Verratti akaikacha PSG majira yajayo ya kiangazi na kocha wa Chelsea, Antonio Conte anavutiwa mno na ‘fundi’ huyo wa dimba la kati (kiungo).

“Hata kama nipo kwenye timu nzuri, kila mchezaji angependa kuichezea Barcelona,” alisema Verratti kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barca usiku wa kuamkia jana.
Licha ya kufukuziwa sana na Chelsea, Verratti ameitaja klabu ambayo angependa kuhamia akiondoka PSG Licha ya kufukuziwa sana na Chelsea, Verratti ameitaja klabu ambayo angependa kuhamia akiondoka PSG Reviewed by Zero Degree on 2/16/2017 05:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.