Mamba mla watu auawa kwa mtego wa kuku mkoani Mwanza
Mamba aliyekula watu wananne katika matukio tofauti mkoani Mwanza ameuawa leo kwa kunaswa na mtego uliowekwa kuku katika eneo la mwalo la Butimba.
Kunaswa na kuuawa kwa mamba huyo kumeibua furaha kwa wakazi wa eneo hilo ambao kwa miaka mitatu iliyopita walilazimika kuchukua tahadhari kila wanapofanya shughuli zao kwenye mwalo huo.
Katibu wa Kitengo cha Kudhibiti na Kuzuia Uvuvi Haramu na Utunzaji wa Mazingira ya Ziwa Victoria (BMU), Robert Charles mamba huyo alinaswa baada ya kuwekewa mtego wa ndoano kwenye kuku eneo la Chuo cha Ualimu Butimba.
“Ni faraja kwetu na kwa wakazi wa eneo hili ambao kwa miaka mitatu sasa wamejawa na hofu ya kuliwa mamba kutokana na watu wanane kukamatwa na kuliwa na mamba huyu,” amesema Charles.
Mwenyekiti wa BMU Kata ya Mkuyuni, Lornard Mpemba amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mamba huyo alikuwa akifika eneo hilo akitokea kisiwa cha Saanane, umbali wa kilometa mbili kutoka eneo mamba alikouliwa.

Reviewed by Zero Degree
on
2/08/2017 06:21:00 PM
Rating: