Loading...

Mashabiki Arsenal washinikiza Uongozi wa klabu kumwachisha kazi Kocha Arsene Wenger

Kipigo ambacho Arsenal ilikipata jana jumamosi ya Februari, 5 kutoka kwa Chelsea cha 3-1 kimemweka kocha wa Arsenal, Arsene Wenger katika kipindi kigumu kufuatia mashabiki wa timu hiyo kushinikiza uongozi wa klabu kumwachisha kazi na kumpa kocha mwingine.

Baada ya mchezo mashabiki wa Arsenal wengi walitumia mitandao mbalimbali ya kijamii kuutaka uongozi wa klabu kumwachisha kazi kwani matokeo ambayo wanayapata hayawaridhishi na wao kama mashabiki wanataka kuona timu yao ikipata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kushinda makombe makubwa.

Katika mtandao wa kijamii wa Twitter, mashibiki wa Arsenal walikuwa wakitumia hashtag ya #Wengerout ili tu kuonyesha umoja wao ni jinsi gani hawahitaji kocha Wenger aendelee kuifundisha timu hiyo.



Aidha kwa upande wa Wenger katika mkutano wake na waandishi wahabari kuelekea mchezo wa Chelsea alisema kuwa tayari uongozi umempa ofa mpya ya kuongeza mkataba na kuendelea kuifundisha klabu hiyo yenye makazi yake jijini London.
Mashabiki Arsenal washinikiza Uongozi wa klabu kumwachisha kazi Kocha Arsene Wenger Mashabiki Arsenal washinikiza Uongozi wa klabu kumwachisha kazi Kocha Arsene Wenger Reviewed by Zero Degree on 2/05/2017 04:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.