Loading...

Mshambuliaji wa Serengeti Boys kapata ‘shavu’ katika klabu hii ya Tunisia

Millardayo ameripoti taarifa nzuri kwa soka la Bongo, ni kuhusu mtanzania Yohana Mkomola anayeichezea timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys ambapo amethibisha kupata dili la kwenda kuichezea club maarufu ya soka ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mkomola aliitwa kwenda kufanya majaribio na timu hiyo amefuzu? mchongo aliupataje? anajibu “Habari hizo ni kweli nilienda Etoile du Sahel kufanya majaribio katika timu yao kwa wiki mbili lakini nilifanya kwa wiki moja na nusu tu nikapata majibu kuwa nimefuzu.”



“Walikuwa wananifatilia maana nilivyomaliza mechi na Congo meneja wangu akaniambia kuwa kuna barua imekuja natakiwa kwenda kufanya majaribio Etoile du Sahel ambapo nitajiunga na kikosi chao cha pili chini ya umri wa miaka 20″ – Yohana
Mshambuliaji wa Serengeti Boys kapata ‘shavu’ katika klabu hii ya Tunisia Mshambuliaji wa Serengeti Boys kapata ‘shavu’ katika klabu hii ya Tunisia Reviewed by Zero Degree on 2/04/2017 01:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.