Mshauri mkuu wa Rais Donald Trump kuhusu usalama wa taifa, Michael Flynn ajiuzulu
Taarifa zinasema mkwe wa Donald Trump, Jared Kushner, (kulia) tayari anatafuta mtu wa kujaza nafasi ya Michael Flynn (kushoto) |
Flynn anadaiwa kujadili vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi akiwa na balozi wa Urusi kabla ya Rais Donald Trump kuingia madarakani.
Anadaiwa kuwapotosha maafisa wa utawala huo mpya kuhusu mazungumzo yake na balozi huyo.
Awali, vyombo vya habari Marekani viliripoti kwamba Wizara ya Haki ilitahadharisha ikulu ya White House mapema kuhusu mawasiliano ya Flynn na maafisa wa Urusi mwishoni mwa mwezi uliopita.
Walisema Bw Flynn huenda akashurutishwa kuwa kibaraka wa urusi.
Maafisa wakuu wa chama cha Democratic walikuwa wametoa wito kwa Bw Flynn kuachishwa kazi.
Mashirika ya habari ya Associated Press na Washington Post yanasema wizara ya haki Marekani ilitahadharisha kuhusu kile ilichosema ni mambo aliyoyasema Bw Flynn kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi.
Ni kinyume cha sheria kwa raia wa kawaida kujihusisha na shughuli za kidiplomasia Marekani.
Mazungumzo kati ya Flynn na balozi wa Urusi yanadaiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana, kabla ya Bw Flynn kuteuliwa kuhudumu katika uatawala wa Bw Trump.
Bw Flynn, ni luteni jenerali mstaafu.
Awali alikana kuzungumza kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi na balozi huyo, na Makamu wa Rais Mike Pence pia alijitokeza hadharani kumtetea.

Bw Flynn baadaye aliambia maafisa wa White House kwamba kuna uwezekano yeye na balozi huyo walizungumzia vikwazo hivyo.
Gazeti la Washington Post lilisema Kaimu Mwanasheria Mkuu Sally Yates aliambia White House kwamba mshauri wao mkuu wa usalama wa taifa "alijiweka katika hali ya hatari" kwa kuzungumza na Warusi kabla yake kuruhusiwa kisheria kufanya hivyo na kwamba Wizara ya Haki ilifahamu kwamba alimpotosha Bw Pence.
Mwezi uliopita, Bi Yates alifutwa kazi na Bw Trump kwa kukataa kutetea marufuku yake dhidi ya raia wa mataifa saba yenye Waislamu wengi kuruhusiwa kuingia Marekani.

Balozi wa Urusi Marekani Sergei Kislyak (kulia), akiwa na rais wa Urusi wakati huo Dmitry Medvedev karibu na Moscow Januari 2009 |
Flynn alipigwa picha na kiongozi wa Urusi Vladimir Putin Decemba 2015 |
Source: BBC Swahili
Mshauri mkuu wa Rais Donald Trump kuhusu usalama wa taifa, Michael Flynn ajiuzulu
Reviewed by Zero Degree
on
2/14/2017 10:37:00 AM
Rating: