Loading...

Wakala wa Rooney alekea China kushugulikia masuala ya uhamisho wa mshambuliaji huyo

Wakala wa Wayne Rooney imepaa kwa ndege kuelekea China ili kujadili suala la uhamisho wa nyota huyo katika baadhi ya klabu kubwa kwenye ligi kuu ya China.

Dirisha la usajili kwa huko China inategemewa kufungwa siku ya Jumanne na klabu za Guangzhou Evergrande, Beijing Guoan, Jiangsu Suning na Tianjin Quanjian ni miongoni mwa klabu zenye nia ya kumsajili Rooney kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo.

Meneja wa Klabu ya Tianjin, Fabio Cannavaro anasema walifanya mchakato wa kutaka kumsajili Rooney lakini katika jitihada zao hawajatoa ofa ya dau walilopanga kuilipa United.

Rooney amekuwa na wakati mugumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha United tangu kuwasili kwa Mourinho pale Old Trafford, amefanikiwa kuanza katika michezo mitatu tu ndani ya miezi miwili iliyopita.

Hajacheza mchezo hata mmoja tangu mwanzoni mwa mwezi Februari kwa sababu ya majeruhi, lakini hivi karibuni ameanza kufanya mazoezi na wenzake kwa mara nyingine tena.
Wakala wa Rooney alekea China kushugulikia masuala ya uhamisho wa mshambuliaji huyo Wakala wa Rooney alekea China kushugulikia masuala ya uhamisho wa mshambuliaji huyo Reviewed by Zero Degree on 2/23/2017 02:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.