Loading...

Yusuf Manji ameachiwa baada ya kudhaminiwa na katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10. Manji alipandishwa kizimbani leo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka la kutumia dawa za kulevya.

Manji amedhaminiwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa. Kabla ya hapo mfanyabiashara huyo alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya moyo yaliyompata baada ya kushikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi Central.

Kocha wa zamani wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa ambaye ni katibu mkuu wa Yanga amemdhamini Mwenyekiti ya Yanga, Yusuf Manji kwa shilingi milioni 10
Kwenye kesi hiyo Manji anashutumiwa kutumia dawa za kulevya aina ya heroin kutokana na vipimo toka kwa Mkemia Mkuu wa serikali. Mshtakiwa amekana kosa hilo.
Yusuf Manji ameachiwa baada ya kudhaminiwa na katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa Yusuf Manji ameachiwa baada ya kudhaminiwa na katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa Reviewed by Zero Degree on 2/16/2017 04:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.