Loading...

Zomea zomea yazuka tena bungeni Dodoma

UAMUZI wa serikali kuhamishia kwenye majengo Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) baadhi ya wizara, uliibua mvutano bungeni jana.

Huku Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akizomewa na wabunge wa upinzani aliposimama kutoa ufafanuzi kuhusu uamuzi huo. 

Wiki iliyopita, serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Anjela Kairuki, ilieleza kuwa baadhi ya wizara zinazohamia Dodoma kutoka Dar es Salaam, ikiwamo wizara yake iliyohamia mjini humo, zitatumia majengo ya Udom kwa muda wakati zikisubiri kujenga ofisi na makazi yake.

Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Idris Kikula jana alisema jumla ya wizara sita zinahamia katika majengo ya chuo hicho. Mvutano ndani ya Bunge jana uliibuka baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Lyimo (Chadema) kutaka serikali ieleza sababu za kubadilisha miundombinu ya elimu kuwa ofisi za serikali.

Source: Nipashe
Zomea zomea yazuka tena bungeni Dodoma Zomea zomea yazuka tena bungeni Dodoma Reviewed by Zero Degree on 2/02/2017 11:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.