Loading...

Jinsi Ashley Cole alivyoikejeli Arsenal

Ikiwa imepita miaka 11 toka aondoke Arsenal,beki wa zamani wa timu hiyo Ashley Cole ameibuka na kuiponda klabu hiyo. Kijembe cha Cole kinakuja wakati ambao mashabiki wa Arsenal wanahitaji faraja kutokana na matokeo mabovu yanayowaandama.

Cole ambaye mwaka 2006 aliwakera sana mashabiki wa Arsenal baada ya kuwaacha kwenye mataa na kufuata pesa za tajiri wa Kirusi Roman Abromovich katika klabu ya Chelsea.

Cole ni kama hajutii kwani amesema kitu pekee anachokumbuka akiwa na Arsenal ni rafiki zake tu na wachezaji wa karibu, lakini anaamini kuondoka kwake Arsenal ndiko kulimsaidi kuchukua karibia makombe yote katika ngazi ya vilabu.

Mbaya zaidi ni pale Ashley Cole alipoulizwa kama huwa anacheka kama akiona Arsenal haifanyi vizuri, akajibu kwa kujiamini Cole alisema “kusema kweli nisiwe muongo, ni kweli huwa nachekaga”.

Cole anasema hajutii akikumbuka alivyoondoka Arsenal na kujiunga na Chelsea. Arsenal wanahangaika sana msimu huu kwani hadi sasa wako nafasi ya 6 ya msimamo wa ligi ya Uingereza na hawana uhakika kuingia katika top four msimu huu.

Ashley Cole kuhamia kwake Chelsea kulimpa kombe la UEFA ambalo hadi sasa Arsenal hawajawahi kulichukua, lakini vilevile Cole alishinda kombe la Uingereza mara nyingi zaidi akiwa na Chelsea.
Jinsi Ashley Cole alivyoikejeli Arsenal Jinsi Ashley Cole alivyoikejeli Arsenal Reviewed by Zero Degree on 3/23/2017 06:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.