Loading...

Kuelekea mechi ya robo fainali ya kombe la shirikisho, Kocha wa Madini aanza vitisho kwa Omog

KOCHA mkuu wa Madini, Abdallah Juma, amemtisha Joseph Omog wa Simba baada ya kusema atahakikisha anaiondoa timu yake katika mchezo wa robo fainali wa Kombe la Shirikisho (FA), itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mjini Arusha.

Juma alisema hawatakubali kuaga kirahisi kwenye michuano hiyo kwa kufungwa na Simba.

Madini inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, Juma alisema wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

“Tutahakikisha tunacheza soka ya ushindani, hivyo Simba wajue wanakuja kukutana na changamoto na hawatapata ushindi kirahisi kwani nasi tunataka kuona tunasonga mbele,” alisema Juma.

Madini walitinga robo fainali baada ya kuwatoa JKT Ruvu kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya bao 1-1.

Simba walitinga robo fainali baada ya kuifunga bao 1-0 African Lyon.
Kuelekea mechi ya robo fainali ya kombe la shirikisho, Kocha wa Madini aanza vitisho kwa Omog Kuelekea mechi ya robo fainali ya kombe la shirikisho, Kocha wa Madini aanza vitisho kwa Omog Reviewed by Zero Degree on 3/13/2017 02:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.