Loading...

Mapato ya mchezo kati ya Madini dhidi ya Simba yaondoka na kigogo Arusha

Meneja wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Jackson Jolwa amesimamishwa kazi na wammiliki wa uwanja huo kwa madai alikuwa hafanyi ipasavyo majukumu yake.

Katibu wa siasa na uenezi wa CCM, Shaaban Mdoe alisema uongozi wa chama hicho ulimsimamisha baada ya mechi ya Madini dhidi ya Simba iliyofanyika uwanjani hapo.

“Wengi wanasema tumemsimamisha kutokana na mapato ya mchezo ule lakini, kinachotakiwa kujulikana kuwa CCM wanapata asilimia 15 ya mapato kwa chochote kinachofanyika hapa, na zoezi hilo husimamiwa na idara ya uchumi,” alisema Mdoe.

Aliongeza kuwa na zoezi la kusimamia mapato kwenye mchezo huo lilipaswa kufanya na mchumi wa chama hicho ambaye siku ya mchezo hakuwepo ndipo aliteuliwa yeye Shaaban Mdoe kulisimamia hilo na siyo kazi ya meneja kusimamia mapato yale.

Akizungumza madai hayo Jackson Jolwa alisema hakuna kosa alilolifanya bali ni ugomvi wao binafsi ndio umesababisha hadi kusimamishwa kazi.

Alisema tatizo hilo lilianza siku ya mchezo wa Madini dhidi ya Simba ambapo katibu mwenezi huyo alitaka aweke vijana wake wasimamie mapato jambo alilipinga kwa madai siyo kazi yao.
Mapato ya mchezo kati ya Madini dhidi ya Simba yaondoka na kigogo Arusha Mapato ya mchezo kati ya Madini dhidi ya Simba yaondoka na kigogo Arusha Reviewed by Zero Degree on 3/24/2017 12:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.