Loading...

Mchakato wa kuhakiki taarifa za wastaafu jijini Dar waanza

Picha ya mtandao
Wizara ya Fedha na Mipango imeanza kuhakiki taarifa za wastaafu waliotumikia Serikali katika utumishi wa umma kwa mkoa wa Dar es Salaam huku ikitoa tahadhari ya kuwafuta wale wote ambao hawatafika kuhakikiwa taarifa zao.

Ukaguzo huo kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2014 na hufanyika kila baada ya miaka miwili, lengo likiwa ni kuboresha taarifa za wastaafu hao katika malipo ya pensheni.

Zoezi hilo kwa awamu hii lilianza Oktoba mwaka jana katika Mkoa wa Pwani.

Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali, Mohamed Mtonga amesema katika mkoa huo, uhakiki umeanza leo (Jumatatu) na utafikia ukomo wake Machi 10 ikiwa ni hatua za mwisho baada ya kumaliza mikoa mingine yote nchini.
Mchakato wa kuhakiki taarifa za wastaafu jijini Dar waanza Mchakato wa kuhakiki taarifa za wastaafu jijini Dar waanza Reviewed by Zero Degree on 3/06/2017 06:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.