Loading...

Mourinho aingia tena vitani kusaka saini ya Mshambuliaji wake wa zamani, Romelu Lukaku

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anapambana na Chelsea katika kuinasa saini ya mshambuliaji wake wa zamani wa timu hiyo, Romelu Lukaku ambaye kwa sasa anakipiga katika Ligi Kuu ya England akiwa na Everton.

Hatua hiyo itakuwa kama vile njia moja ya Mourinho kukubali kosa lake baada ya kumuuza staa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kwenda Everton akiwa na Chelsea katika dirisha kubwa la majira ya joto mwaka 2014.

Mourinho ameingia sokoni kusaka mshambuliaji wa kusaidiana na staa wake, Zlatan Ibrahimovic huku akimruhusu Wayne Rooney kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia klabu hiyo tangu mwaka 2004 kwa mafanikio makubwa.
Mourinho aingia tena vitani kusaka saini ya Mshambuliaji wake wa zamani, Romelu Lukaku Mourinho aingia tena vitani kusaka saini ya Mshambuliaji wake wa zamani, Romelu Lukaku Reviewed by Zero Degree on 3/30/2017 07:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.