Loading...

Msanii wa muziki wa Taarabu nchini, Khadija Kopa ana haya ya kusema kwa BASATA

Mama wa mipashao Khadija Kopa ana jambo limemkaa rohoni kwa muda mrefu sana na angependa liwafikie wahusika.

Msanii huyo mkongwe wa muziki wa Taarab alifunguka jinsi ambavyo anaumizwa na mwenendo wa muziki huo nchini, kwa maneno yake; “sisi tunaumiza vichwa sana lakini muziki wetu unapotea…“ akidai yote ni kutokana na BASATAkushindwa kufanya kazi yao ya kuwasimamia wasanii wa muziki wa Taarab ipasavyo.

” BASATA wanatusajili sisi, tunalipa ada zetu kwa ajili ya BASATA lakini hawatusimamii. Sisi tunaumiza sana vichwa kwenye kazi hizi ila kuna watu wanaunda mabeni kwa ajili ya kupiga viingilio bia na nyimbo hizi hizi zetu… muziki wetu unapotea. Hivyo naona kama vile BASATA hawawezi kutusimamia maana tumeshaomba sana juu ya mambo haya lakini wameshindwa hivyo ninaiomba Serikali, Wizara na Waziri watusaidie kuhusu habari ya nyimbo zetu.” – Khadija Kopa.

Akaendelea kusema…

“Mambo mengine wanafuatilia… utasikia mtu ametoa wimbo mbaya anafungiwa lakini mbona hawashughuliki kwa haya mambo mengine, mengine mbona hawafuatili? Sasa kuna haja gani ya kukaa Serikalini na kuchukua mishahara?”Khadija Kopa.

Source: Global Publishers
Msanii wa muziki wa Taarabu nchini, Khadija Kopa ana haya ya kusema kwa BASATA Msanii wa muziki wa Taarabu nchini, Khadija Kopa ana haya ya kusema kwa BASATA Reviewed by Zero Degree on 3/06/2017 03:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.