Loading...

Simba SC kuungana na Juventus ya Italia

Bilionea kijana zaidi barani Afrika, Mohammed Dewji maarufu kama Mo, ametua nchini Italia na kufanya ziara katika klabu bingwa ya nchini humo, Juventus.

Juventus maarufu kama “Vibibi Kizee vya Turin”, ndiyo timu yenye mafanikio makubwa zaidi kwa kipindi zaidi nchini humo licha ya kuwepo kwa timu nyingine za AC Milan na Inter Milan ambazo zinaonekana kudorora.



Akizungumza kutoka Turin, Italia, Mo Dewji amesema kwamba alifanya ziara hiyo na Juventus wameonekana wako tayari kuendeleza mchezo wa soka kwa kuwekeza nchini Tanzania.

“Wiki hii nilifanya kikao na Juventus FC. Wanayo nia ya kuendeleza soka kwa vijana wa Tanzania. Ninatazamia kuitambulisha timu hiyo ya Italia kwa uongozi wa Simba SC ili waanze majadiliano ya jambo hilo,” alisema Mo.

Mo alisema mambo mengi waliyozungumza ni mchakato, hivyo ni suala la kuangalia na huenda atazungumzia zaidi hapo baadaye.

Juventus ni moja ya klabu yenye mfumo bora kabisa wa ukuzaji wa wachezaji vijana. Pia inashirikiana na baadhi ya klabu kubwa za barani Afrika lakini nyingi ni zile kutoka Afrika Kaskazini hasa katika nchi za Libya (wakati ikiwa tulivu), Tunisia, Morocco na Misri.

Kama Simba itapata bahati hiyo, itakuwa imepata nafasi nzuri ya kujiendeleza na kujifunza mengi kibiashara na kimaendeleo kupitia Juventus, pia maarufu kama Juve.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Ltd, ni mwanachama, shabiki na aliwahi kuwa mfadhili wa Simba kwa kipindi kirefu cha mafanikio.

Lakini kwa sasa, Mo Dewji ameendelea kuifadhili Simba na imeelezwa kila mwezi amekuwa akitoa takribani au zaidi ya Shilingi milioni 100 katika ulipaji mishahara na mambo mengine ya motisha kwa wachezaji.
Simba SC kuungana na Juventus ya Italia Simba SC kuungana na Juventus ya Italia Reviewed by Zero Degree on 3/25/2017 05:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.