Loading...

VIDEO: Vanessa Mdee akishirikishwa na msanii toka Nigeria, Orezi

Siku mbili zilizopita Vanessa Mdee alitweet kuwa kuna wimbo mpya unakuja wiki hii, na kama ulikuwa standby kupokea kazi mpya kutoka kwa Vee Money ikamate hii.

Kupitia Instagram page yake Vanessa Mdee amepost teaser ya wimbo huo unaoitwa ‘Just Like That’ ikiwa ni kazi aliyoshirikishwa na msanii kutoka Nigeria Orezi. Watayarishaji wa wimbo huu ni Popito na Dr. Amir, Director wa video ni Seasan kutoka Nigeria.

Kwa wale wanaotafuta sababu za kwenda club Ijumaa hii basi wimbo huu ni sababu ya kukupa vibe la kutosha.

” When I move you move, Just Like That, Just Like That… When I move you move Just Like That, Just Like That…” – Orezi na Vanessa wanaimba kwa kupokezana, huku Vee akiendelea kuimba – “ Nami nimo wengine usiowaone, kuwa na mimi pekee, kwenye vita nitetee… kuwa na mimi pekee,kwenye vita nitetee…“


VIDEO: Vanessa Mdee akishirikishwa na msanii toka Nigeria, Orezi VIDEO: Vanessa Mdee akishirikishwa na msanii toka Nigeria, Orezi Reviewed by Zero Degree on 3/17/2017 04:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.