Loading...

Wakimbizi watatu wamekatwa kambini wakiwa na bomu

Jeshi la polisi mkoani Kigoma, limewakamata wakimbizi watatu kutoka nchini Burundi wanaohifadhiwa katika kambi ya wakimbizi Mtendeli katika wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wakiwa na bomu moja la kutupwa kwa mkono pamoja na mali kadhaa za wizi walizopora baada ya kuteka magari katika barabara ya Kakonko- Kasulu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema katika siku za hivi karibuni kumeibuka matukio ya utekaji na uporaji wa kutumia silaha huku baadhi ya wakimbizi wakituhumiwa kujihusisha na ujambazi hali iliyolilazimu Jeshi la polisi kufanya oparesheni katika kambi hiyo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu na mali kadhaa za wizi pamoja na zana wanazotumia katika uhalifu na kwamba bomu litakabidhiwa kwa Jeshi la wananchi wa Tanzania ili liharibiwe.

Kwa upande wake Mkuu wa kambi ya wakimbizi Mtendeli Innocent Mwaka akizungumzia hali ya usalama katika kambi hiyo,amesema serikali haijaridhishwa na kuwepo kwa wahalifu katika kambi hiyo na kwamba wataendelea kuwasaka wakimbizi wote wanaojihusisha na uhalifu.

Source: ITV
Wakimbizi watatu wamekatwa kambini wakiwa na bomu Wakimbizi watatu wamekatwa kambini wakiwa na bomu Reviewed by Zero Degree on 3/02/2017 04:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.