Loading...

Waziri wa Elimu akiri kusikitishwa na utendaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi [VETA]

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema amesikitishwa kuona Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(Veta) bado haijatambua dhana ya uwajibikaji kwa kuzingatia matokeo ya kazi.

Profesa Ndalichako amesema inasikitisha kuona kuwa wanapokaribia kuingia robo ya mwisho wa mwaka wa fedha 2017/18 karibu miradi yote ya Veta haijaanza kutekelezwa.

"Miradi iliyotekelezwa ni ile ya kujenga uwezo,mafunzo lakini siyo ya ujenzi wa Veta ambazo zinahitajika sana kwa vijana wetu,"amesema Profesa Ndalichako.
Waziri wa Elimu akiri kusikitishwa na utendaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi [VETA] Waziri wa Elimu akiri kusikitishwa na utendaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi [VETA] Reviewed by Zero Degree on 3/06/2017 03:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.