Akamatwa uchi akiwa anawanga kwenye njia panda 3 mida ya mchana
MKAZI wa kitongoji cha Ngorongoro kata ya Mikumi C wilayani Kyela mkoani Mbeya (jina linahifadhiwa) amenusurika kufikishwa polisi na wananchi waliomkamata akizoa mchanga kwenye makutano ya barabara tatu akiwa uchi.
Juma Athuman ambaye ni mkazi wa Kyela alisema mkazi huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika kijiji cha Itunge.
Alisema walipata taarifa za kuwapo kwa mtu huyo kutoka wa watoto waliokuwepo eneo hilo.
Alisema kijana huyo alifika katika makutano ya njia tatu hizo akiwa na baiskeli, akaiegesha pembezoni mwa barabara ya Mikumi-Itunge kisha kuingia kwenye kichaka kilicho jirani na mavazi kamili.
Baada ya muda mfupi, alisema Athuman, kijana huyo alirudi barabarani akiwa mtupu na kuanza kuchota mchanga na kuuweka kwenye mfuko wa 'rambo', na wakati akitaka kuondoka ndipo watu wakajitokeza na kumkamata.
Shuhuda mwingine wa tukio hilo, Asha Ismail alisema wananchi walitaka kumpeleka polisi lakini baada ya mashauriano walikubaliana kwa kuwa alikuwa akifanya mambo yake ya ushirikina, aamriwe kurudisha mchanga na kuondoka.
Alisema vitendo vya kishirikina wilayani humo vimeendelea kuchukua sura mpya baada ya siku za hivi karibuni jeshi la polisi kuwahi kumkamata kijana mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji akiwa na maji yaliyotumika kuoshea maiti, yakiwa kwenye dumu la lita tano ambayo alisema anakwenda kutengenezea dawa.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Ibrahim Mwakanyamale alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini hakushuhudia kwa kuwa alikuta mtu huyo ameachiwa.

Source: Nipashe
Akamatwa uchi akiwa anawanga kwenye njia panda 3 mida ya mchana
Reviewed by Zero Degree
on
4/25/2017 04:31:00 PM
Rating: