Alphonce Simbu awa mshindi wa 5 katika mbio za London Marathon
Mwanariadha kutoka Tanzania Alphonce Simbu, Jumapili hii amemaliza kama mshindi wa tano katika mbio za London Marathon nchini Uingereza.
Inaonyesha anayeshika nafasi ya tano katika mashindano hayo anaibuka na kitita cha dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 22).
Alphonce ambaye ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Mumbai Marathon, amewapa wakati mgumu manguli wa riadha ulimwenguni walioshiriki mbio hizo za London akiwemo Muethiopia Kenenisa Bekela pamoja wa wengine kutoka Ethiopia na Kenya.
Ushindi huu ni mkubwa kwa Tanzania na tunampa pongezi Alphonce Simbu kwa kufikia hatu hii kubwa na kwa kuipepeprusha bendera ya nchi yetu vyema.
Ushindi huu ni mkubwa kwa Tanzania na tunampa pongezi Alphonce Simbu kwa kufikia hatu hii kubwa na kwa kuipepeprusha bendera ya nchi yetu vyema.
Hata hivyo, Simbu ambaye alianza vibaya alilazimika kubadili gia mwishoni na kuwashinda zaidi ya Wakenya sita na Waethiopia wawili, Mganda mmoja ili kushika nafasi hiyo ya tano.
Alphonce Simbu awa mshindi wa 5 katika mbio za London Marathon
Reviewed by Zero Degree
on
4/23/2017 08:10:00 PM
Rating: