Loading...

Jinsi mkutano wa Cuf ulivyovamiwa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha

Watu wasiofahamika wakiwa na bastola wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF upande unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Vina, Mabibo, ulipangwa kuanza leo saa tano asubuhi lakini kabla haujaanza watu waliovalia soksi nyeusi usoni(mask) walivamia na kuanza kuwapiga wanachama wa CUF na waandishi waliokuwa kwenye mkutano huo.

Wananchi wamshambuliwa Mvamizi mmoja:

Mtu mmoja miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka. 

Mtu huyo, ambaye hajafahamika alikuwa akitoroka pamoja na wenzake katika eneo hilo la Vina Hotel Mabibo mara baada ya kutekeleza uvamizi huo katika mkutano wa wanachama wa CUF.

Watu hao waliovamia mkutano huo, walikuwa na bastola.

Polisi wawasili eneo la tukio:

Polisi inawahoji wanachama wa CUF waliovamiwa na watu waliovaa ‘mask’ katika ukumbi wa Vina Hoteli, Mabibo leo.

Polisi imeshafika eneo la tukio na inawahoji wanachama hao w wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad waliokuwa wakifanya mkutano wao wa ndani.

Pia Polisi inawahoji waandishi wa habari waliopo eneo la tukio.

Inaelezwa kuwa watu wanne, waliovaa soksi nyeusi usoni (mask) walivamia mkutano huo wa CUF wakiwa na mapanga na bastola. 
Jinsi mkutano wa Cuf ulivyovamiwa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha Jinsi mkutano wa Cuf ulivyovamiwa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha Reviewed by Zero Degree on 4/22/2017 02:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.