Loading...

Kuna mipango ya kutaka kukifuta chama chetu, Lipumba

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF anayetambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba, ameandika barua maalumu kwa Jukwaa la Wahariri Tanzania kuonesha kusikitishwa na vurugu zilizotokea katika mkutano wa CUF uliosababisha waandishi kufanyiwa fujo.

Akizungumza katika mahojiano na mtangazaji wa Azam Two, Prof. Lipumba ameliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo huku akimtaka Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif wakae wazungumze ili wamalize tofauti zao na wakijenge chama:

“Baada ya kulisikia hilo niliamua kuchukua jukumu la kuwaandikia Jukwaa la wahariri barua ambayo ipo mbioni kwenda kwenye ofisi zao kwamba mimi binafsi kama mwenyekiti wa CUF nalaani kitendo cha kupigwa kwa waandishi wa habari na nijambo ambalo hatulikubali kabisa, hatuwezi kujenga Demokrasia ikiwa waandishi wahabari hawafanyi kazi yao katika hali ya amani na utulivu.

“Vile vile kijana wetu amekatwa kisigino kwa panga na anavyo elewa yeye kijana aliyemkata anaitwa Mohamedi Mgonvi na taarifa hii imepelekwa kwenye vyombo vya dola kwaiyo vyombo vya dola inalishughulikia na tulitoa wito ambao ulitolewa na Mkurugenzi wetu wahabari na uwenezi.''
Kuna mipango ya kutaka kukifuta chama chetu, Lipumba Kuna mipango ya kutaka kukifuta chama chetu, Lipumba Reviewed by Zero Degree on 4/28/2017 09:29:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.