Loading...

Takukuru imeokoa zaidi ya milioni 90 kama mishahara hewa

Mkuu wa Takukuru mkoani Ruvuma, Yustina Chagaka 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) Mkoa wa Ruvuma, imeokoa Sh 91,811,768 kama mishahara hewa. Fedha hizo ni kuanzia Julai 2016 hadi Machi mwaka huu. Kati ya fedha hizo, katika sekta ya elimu imeokoa Sh 61,078,460 na sekta ya kilimo ni Sh milioni 2.233.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Takukuru mkoani Ruvuma, Yustina Chagaka wakati akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kuanzia Julai 2016 hadi Machi mwaka huu kwa waandishi wa habari mjini Songea. Chagaka alibainisha kuwa Sh milioni 28.50 zimeokolewa katika sekta ya ujenzi zilizolipwa kwa mkandarasi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Mpitimbi B hadi Mbinga Mhalule katika halmashauri ya wilaya ya Songea kwa kazi ambazo hazikufanyika, mkandarasi aliamuliwa kurejesha fedha hizo.

Aidha, alisema katika kipindi hicho Takukuru mkoa imepokea taarifa 173 kutoka kwa wananchi kupitia vyanzo mbalimbali ambapo idara zinazolalamikiwa na idadi ya kesi kwenye mabano ni Tamisemi (40), Elimu(26), Kilimo( 21), Afya(18), Ujenzi(17), Ardhi(16), Mahakama (14), Maji (10), Polisi(9) na watu binafsi malalamiko mawili. Chagaka alisema Takukuru katika kipindi hicho imeweza kufanya kazi za udhibiti sita ambapo katika wilaya ya Songea zimefanyika udhibiti nne kuhusu mianya ya rushwa na upendeleo katika uteuzi wa kaya maskini zinazonufaika na Mpango wa Tasaf 111 wa kusaidia kaya masikini.
Takukuru imeokoa zaidi ya milioni 90 kama mishahara hewa Takukuru imeokoa zaidi ya milioni 90 kama mishahara hewa Reviewed by Zero Degree on 4/26/2017 07:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.