Watuhumiwa wa mauaji ya viongozi wa vijiji na askari mkoani Pwani wameuawa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Oesmo Lyanga |
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, ONESMO LYANGA amesema katika taarifa yake kuwa watu hao wamefariki dunia wakati wakipelekwa hospitali ya Mission ya Mchukwi kwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwa risasi miguuni na kiunoni walipojaribu kukimbilia porini wakiwa kwnye pikipiki baada ya kukaidi amri halali ya polisi iliyowataka wasimame kutokana na kuwatilia mashaka.
Amesema polisi waliokuwa katika doria walipata taarifa kutoka kwa wa safiri kuwa waliona pikipiki tatu zilizokuwa zinatokea Kibiti kupitia barabara kuu ya Dar es salaam -Lindi zimepakia watu watatu kila mmoja na pikipiki mbili kati ya hizo ziliwabeba waliovalia hijabu ndipo walipowapa taarifa askari wa usalam barabararni walioko katika kizuizi cha Mparange ili wawasimamishe na kuwatambua lakini hawakutii.
Amesema askari wa kituo cha Mwembe, Muhoro waliwasimamisha lakini hawakutii amri na kuongeza kasi, ndipo askari waliwafuatilia hadi kuvuka daraja la Mkapa na wakatoa onyo kwa kufyatua risasi hewani lakini waliendelea kukaidi.
Amesema baadaye watu hao waliamua kuruka kutoka kwenye pikipiki zao na kukimbilia msituni, kitendo kilichowafanya polisi kuwafyatulia risasi za miguuni na kiunoni na kuwakamata lakini walifariki dunia wakati wakikimbizwa hospitali ya Mission ya Mchukwi ambako daktari alithibitisha watu hao walikuwa wameshafariki.
Kamanda amesema majeruhi hao waliovalia hijabu baadaye walitambuliwa kuwa walikuwa wanaune waliotumia pikipiki aina ya BOXER yenye namba za usajili MC 272 BLW.
Source: ITV

Reviewed by Zero Degree
on
4/22/2017 05:36:00 PM
Rating: