Yanga kuikosa huduma ya Bossou na Donald Ngoma leo
YANGA itawakosa nyota wake, Vicent Bossou na Donald Ngoma kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi alisema Ngoma aliumia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mc Algiers na Bossou anaumwa na juzi alishindwa kuendelea na mazoezi.
“Tusahau matokeo ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuondolewa na MC Algers, tunarudi nyumbani na Tanzania Prisons ni timu ya muda mrefu kwenye ligi na wapo vizuri kwenye msimamo wa ligi, hivyo hatuwadharau,”alisema Mwambusi.
Yanga ilitolewa katika hatua ya mchujo ya kufuzu kwa makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufungwa 4G na hivyo kutoka kwa kipigo cha jumla ya mabao 4-1 kufuatia ushindi wa 1-0 katika mchezo wa awali.
Pia Mwambusi alisema wamejiandaa kuhakikisha wanashinda mchezo huo, kwani ili kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Afrika ni lazima uwe bingwa wa ligi au bingwa wa Kombe la Shirikisho.
Mchezo huo utatoa mshindi ambaye ataungana na timu za Mbao, Simba na Azam FC, ambazo tayari zimefuzu kwa hatua ya nusu fainali. Azam FC ilikata tiketi ya kucheza nusu fainali baada ya kuifunga Ndanda FC mabao 3-1, kwenye Uwanja wa Azam na Mbao iliifunga Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Kagera, wakati Simba iliwatoa Madini ya Arusha kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Nusu fainali inatarajiwa kufanyika baada ya droo itakayochezeshwa kesho katika kituo cha Televisheni cha Azam mubashara. Bingwa wa michuano hii ambayo msimu huu ilishirikisha timu 86 kuanzia mabingwa wa mikoa (22), ligi daraja la pili (24), ligi daraja la kwanza (24) na Ligi Kuu (timu 16), atazawadiwa Sh Milioni 50 na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho - CAF.

Reviewed by Zero Degree
on
4/22/2017 01:35:00 PM
Rating: