Alichosema 'Cannavaro' baada ya Yanga kufungwa na Mbao FC
Nahodha wa klabu ya Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amekiri wapinzani wao walitumia nafasi yao vizuri na kuji hakikishia Ushindi waliopata, baada ya Mchezo kumalizika dhidi ya Mbao FC.
Nahodha huyo amewataka mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kuelekeza nguvu yao katika ligi, kwa sababu bado wana nafasi ya kuiwakilisha nchi katika anga za kimataifa kupitia Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom.
Nae nahodha wa klabu ya Mbao Fc Ndikumana , amekiri kuwa Yanga ni timu nzuri, ila ushindi wao unatokana na Umoja waliokuwa nao ndani ya klabu na hivyo ndivyo watakavyocheza hata wakikutana na klabu ya Simba Sc.
Katika mchezo huo, klabu ya soka ya Yanga imevuliwa taji la pili msimu huu, baada ya kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inayojulikana kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), kufuatia kipigo cha 1-0 wao wakiwa ndio Mabingwa watetezi Mchezo uliopigwa katika Dimba la CCM Jijini , Mwanza.
“Tumejitahidi kwenye Game lakini wenzetu wamepata nafasi, wameitumia na hii ndio Football, ila tunajipanga upya na tunakubali matokeo”,”This is Football kwa sababu wametengeneza nafasi na ikapatikana ushindi, so huwezi kuulaumu sana”.
Nahodha huyo amewataka mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kuelekeza nguvu yao katika ligi, kwa sababu bado wana nafasi ya kuiwakilisha nchi katika anga za kimataifa kupitia Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom.
Nae nahodha wa klabu ya Mbao Fc Ndikumana , amekiri kuwa Yanga ni timu nzuri, ila ushindi wao unatokana na Umoja waliokuwa nao ndani ya klabu na hivyo ndivyo watakavyocheza hata wakikutana na klabu ya Simba Sc.
Katika mchezo huo, klabu ya soka ya Yanga imevuliwa taji la pili msimu huu, baada ya kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inayojulikana kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), kufuatia kipigo cha 1-0 wao wakiwa ndio Mabingwa watetezi Mchezo uliopigwa katika Dimba la CCM Jijini , Mwanza.
Alichosema 'Cannavaro' baada ya Yanga kufungwa na Mbao FC
Reviewed by Zero Degree
on
5/02/2017 12:32:00 AM
Rating: